KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA NG’OMBE
Ng’ombe wanafugwa kwa ajili ya nyama na
maziwa lakini pia hutoa mazao mengine kama ngozi,mbolea na hutumika kama
wangyama kazi. Zaidi ya asilimia95 ya ng,ombe na hutumika kama wanyama
kazi. Zaidi ya asilimia 95 ya ng’ombe wanaofugwa hapa nchini ni wa
asili ambao huzalisha nyama na maziwa kwa kiwango kidogo ikilinganishwa
na wale wachache walioboreshwa. Ng’ombe walioboreshwa wamegawanyika
katika makundi mawili, wale wanaofugwa kwa ajili ya nyama na wanaofugwa
kwa ajili ya maziwa. Ili kuwawezesha ng’ombe kuzalisha mazao bora ya
nyama, maziwa na ngozi mfugaji anapaswa kufuata kanuni za ufugaji bora
ambazo ni pamoja na:-
i) Kufuga ng’ombe katika eneo kwa kuzingatia uwianao wa idadi ya ng’ombe na malisho katika mfumo wa ufugaji huria.
ii) Kujenga banda au zizi bora.
iii) Kuchagua koo/aina ya ng’ombe kulingana na uzalishaji (nyama au maziwa).
iv) Kutunza makundi mbalimbali ya ng’ombe kulinga na umri na hatua ya uzalishaji.
v) Kumpa ng’ombe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili.
vi) Kudhibiti magonjwa ya ng’ombe kama inavyoshauriwa na mtaalamu wa mifguo.
vii) Kuvuna mifugo katika umri na uzito muafaka kulingana na mahitaji ya soko.
viii) Kuzalisha maziwa, nyama na ngozi zinazokidhi viwango vya ubora na usalama.
ix) Kutunza kumbukumbu za uzalishaji na matukio muhimu ya ufugaji.
MIFUMO YA UFUGAJI
Ng’ombe wanaweza kufugwa katika mfumo wa
ufugaji huria au kulishwa katika banda (ufugaji shadidi). Ufugaji huria
huhitaji eneo kubwa la ardhi yenye malisho mazuri na vyanzo vya
maji. Pamoja na kuwa na ufugaji huu, ni muhimu ardhi hiyo itunzwe kwa
kuzingatia uwiano wa idadi ya ng’ombe na malisho. Ufugaji wa shadidi
uzingatie uwepo wa banda bora na lishe sahihi.
UFUGAJI KATIKA MFUMO HURIA
Ili mfugaji aweze kupata mazao mengi na bora katika ufugaji huria anapaswa kuzingatia yafuatayo:-
- Atenge eneo la kutosha la kufugia kulingana na idadi ya ng’ombe alionao.
- Atunze malisho ili yawe endelevu na yapatikana wakati wote.
- Awe na eneo lenye maji ya kutosha na
- Atenganishe madume na majike ili kuzuia ng’ombe kuzaa bila mpangilio.
Matunzo mengine ya ng’ombe yazingatie vigezo vingine muhimu kama umri hatua ya uzalishaji na matumizi ya ng’ombe husika.
BANDA/ZIZI BORA LA NG’OMBE
BANDA BORA.
Band alijengwe sehemu ya mwinuko mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa zifuatazo:-
· Uwezo wa kumkinga ng’ombe dhidi ya mvua, upepo, jua kali na baridi.
· Kuta imara zenye matunda au madirisha kwa ajili ya kuingiza hewa na mwanga wa kutosha,
· Sakafu yenye mwinuko upande mmoja ili isiruhusu maji na uchafu kutuama.
· Lijengwe
katika hali ya kuruhusu kufanyiwa usafi kwa urahisi kila siku, na
sakafu ngumu ya zege au udongo ulioshindiliwa na kuweka malalo.
· Paa lisilovuja na
Aidha kwa wafugaji wanaofuga katika ufugaji huria ambako mazizi hutumika, inashauriwa kuzingatia yafuatayo:-
· Zizi likae mahali pa mwinuko pasiporuhusu maji kutuama.
· Zizi liweze kukinga mifugo dhidi ya wezi na wanyama hatari.
· Ukubwa wa zizi uzingatie idadi na umri wa mifugo ng’ombe watengwe kulingana na umri wao.
· Zizi lifanyiwe usafi mara kwa mara na
· Liwe
na sehemu ya kukamulia (kwa ng’ombe wa maziwa), stoo ya vyakula, sehemu
ya kutolea huduma za kinga na tiba, eneo la kulishia na maji ya kunywa.
ZIZI BORA
Zizi lijengwe sehemu ya mwinuko isiyoruhusu maji kutuama mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa zifuatazo:-
§ Liweze kuhakikisha usalama wa ng’ombe.
§ Ukubwa wa zizi uzingatie idadi ya mifugo.
§ Liwe na sakafu ya udongo ulioshindiliwa vizuri na kufanyiwa usafi mara kwa mara
§ Zizi la ndama liwe na paa ma
§ Lijengwe kwa vifaa madhubuti na visivyoharibu ngozi.
UCHAGUZI WA KOO NA AINA YA NG’OMBE WA KUFUGA
Kwa ufugaji wenye tija, mfugaji anashauriwa kuchagua koo na aina ya ng’ombe kwa kuzingatia malengo ya ufugaji (nyama au maziwa).
NG’OMBE WA NYAMA
Ng’ombe wanaofaa kufugwa kwa ajili ya
uzalishaji nyama ni wale wanaokua kwa haraka na kuweka misuli mikubwa
iliyojengeka vizuri. Baadhi ya koo zenye sifa hizo ni pamoja na Boran,
Mpwapwa (nyama na maziwa), Charolais, Aberdeen Angus, pamoja na chotara
wao. Hata hivyo, nchini Tanzania ng’ombe aina ya Zebu (mfano
Ufipa,Gofo, Masai, Sukuma, Tarime, Iringa red), Sanga (Ankole) na
chotara wao ndio hutumika kama ng’ombe.
NG’OMBE WA MAZIWA.
Sifa za ng’ombe wa maziwa zifuatazo:-
- Umbo lililopanuka kwa nyuma na kupungua kuelekea kichwani.
- Mgongo ulionyooka kuanzia mabegani kuelekea mkiani
- Miguu ya nyuma mirefu iliyonyooka, minene yenye kuacha nafasi kwa ajili ya kiwele na kwato imara.
- Kiwele kiwe kikubwa chenye chuchu nne, ndefu na unene wa wastani
- Nafasi kati ya chuchu na chuchu iwe ya kutosha na
- Endapo ng’ombe anakamuliwa awe na kiwele kikubwa kilichoshikamana vizuri mwilini, na mishipa mikubwa kwenye kiwele iliyosambaa.
Aina ya ng’ombe wa maziwa wanaofugwa kwa
wingi nchini ni pamoja na Friesian, Ayrshire, jersey, Mpwapwa, Simmental
na chotara watokanao na mchangoayiko wa aina hizo na Zebu.
UTUNZAJI WA MAKUNDI MABALIMBALI YA NG’OMBE WA MAZIWA KULINGANA NA UMRI NA HATUA YA UZALISHAJI
UTUNZAJI WA NDAMA
Mfugaji anapaswa kutunza ndama vizuri kwa
lengo la kupata ng’ombe wengi na bora kwa ajili ya maziwa. Mambo
muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ndama tangu kuzaliwa hadi
kuachishwa maziwa ni pamoja na
- Kuhakikisha
kuwa ndama anapakwa dawa ya kuzuia maambukizi ya viini ya magonjwa
kupitia kwenye kitovu, kwa mfano dawa joto (Tincute of Iodine) mara
baada ya kuzaliwa na
- Ndama
apatiwe maziwa ya awali yaani dang’a (colostrums) mara baada ya
kuzaliwa kwa lengo la kupata kinga ya mwili dhidi ya magonjwa. Aidha,
aendelee kunyonya maziwa hayo kwa muda wa siku 3-4.
Endapo jike aliyezaa amekufa au hatoi
maziwa, apewe dang’a toka kwa ng’ombe mwingine kama yupo au dang’a
mbadala, ambayo inaweza kutengenezwa kwa kuchanganya vitu vifuatavyo:-
- Lita moja ya maziwa yaliyokamuliwa wakati huohuo.
- Lita moja ya maji yaliyochemshwa na kupozwa hadi kufikia joto la mwili.
- Kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya samaki (cod liver oili).
- Mafuta ya nyonyo vijiko vya chai 3 na
- Yai moja bichi
Koroga mchanganyiko huo, weka katika
chupa safi na ndama anyweshwe kabla haujaopoa. Ndama anyweshwe
mchanganyiko huo mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 3 mfululizo na kila
mara mchanganyiko uwe mpya. Wakati wa kunywesha chupa iwekwe juu
ya kidogo ili asipaliwe.
- Endapo
ndama hawezi kunyonya ng’o mbe akamuliwe na ndama anyweshwe maziwa kwa
njia ya chupa kwa kuzingatia usafi wa maziwa na chupa.
- Ndama aendelee kunyweshwa maziwa kwa kiasi kama ilivyoonyeshwa kwenye Jedwali Na. 1
- Ndama aanze kuzoeshwa kula nyasi laini, pumba kidogo na maji safi wakti wote kuanzia wiki ya 2 baada ya kuzaliwa na
- Ndama
aachishwe kunyonya au kupewa maziwa akiwa na umri wa miezi 3. Mfugaji
ahakikishe kwamba ndama anayeachishwa kunyonya ana afya nzuri.
JEDWALI NA. 1 KIASI CHA MAZIWA NA CHAKULA MAALUMU KWA NDAMA
UMRI (WIKI)
|
KIASI CHA MAZIWA KWA SIKU (LITA)
|
KIASI CHA CHAKULA MAALUM CHA NDAMA KWA SIKU (KILO)
|
1
|
3.0
|
0.0
|
2
|
3.5
|
0.0
|
3
|
4.0
|
0.0
|
4
|
4.5
|
0.0
|
5
|
5.0
|
0.1
|
6
|
5.0
|
0.2
|
7
|
5.0
|
0.3
|
8
|
4.0
|
0.4
|
9
|
3.0
|
0.7
|
10
|
2.0
|
1.0
|
11
|
1.5
|
1.25
|
12 - 16
|
0.75
|
1.5
|
Vyombo vinavyotumika kulishia ndama visafishwe vizuri kwa maji yaliyochemshwa, sabuni na kukaushwa.
Matunzo mengine ya ndani ni pamoja na:-
- Kuondoa pembe kati ya siku 3 hadi 14 mara zinapojitokeza ili kuzuia wanyama kuumizana na kuharibu ngozi,
- Kukata chuchu za ziada kwa ndama jike
- Kuhasi
ndama dume wasiozidi umri wa miezi 3 ambao hawatahitajika kwa ajili
kuendeleza kizazi ili wakue hawatajika kwa ajili ya kuendelea kizazi ili
wakue haraka na kuwa na nyama nzuri.
- Kuweka
alama au namba za utambulisho kati ya siku ya kwanza na ya tano, mfano
kuvalishwa hereni kwenye masikio kwa ajili ya urahisi wa udhiti wa
umiliki na utunzaji kumkukumbu na,
- Kuwapatia kinga dhidi ya maabukizi na tiba ya magonjwa wanapougua.
Huduma hizi zifanyike chini ya maelekezo ya mtaalam wa mifugo.
UTUNZAJI WA NDAMA BAADA YA KUACHISHWA MAZIWA HADI KUPEVUKA (MIEZI – 18)
- Ndama baada ya kuachishwa maziwa apate malisho bora na chakula mchanganyiko kuanzia kilo 2 4 kwa siku kutegemea umri wake na
- Ndama wanapofikia umri wa miezi 18 wachaguliwe wanaofaa kuendeleza kizazi, wasio na sifa nzuri waondolewe katika kundi
.
UTUNZAJI WA MTAMBA
Mtamba ni ng’ombe jike aliyefisha umri wa
kupandwa (wastani wa miezi 18) hadi anapozaa kwa mara ya kwanza. Ni
muhimu kutunza vizuri mtamba ili kupata kundi bora la ng’ombe. Miezi 3
kabla ya kupandishwa mtamba apatiwe:-
- Malisho bora
- Maji ya kutosha
- Madini mchanganyiko na
- Chakula cha ziada kiasi cha kilo 2 – 3 kwa siku, ili kuchochea upevukaji na kuongeza uzito wa mwili.
UTUNZAJI WA NG’OMBE WAKUBWA
Kundi hili linajumuisha ng’ombe wenye mimba, wanaokamuliwa na madume. Mfugaji anapaswa kutunza vizuri ng’omb
No comments:
Post a Comment