Monday, July 11, 2016

AINA YA NG'OMBE BORA WA MAZIWA

AINA YA NG'OMBE BORA WA MAZIWA



Uzalishaji wa maziwa ni biashara nzuri sana na ya kuvutia ambayo huwa na faida nyingi na humfanya mfugaji kuridhika hasa kwa yule anayependa kazi hii. Hata hivyo, ni lazima kuanza kwa kuweka msingi imara hata kabla ya kufikiria ni aina gani ya mbegu utaichukua kwa ajili ya kufuga. Ni vizuri kufahamu kuwa, usimamizi ni moja ya jambo muhimu sana ambalo likifanyiwa uzembe linaweza hata kumbadilisha ng’ombe wa maziwa kuwa na uzalishaji duni kama ngo’mbe wa kienyeji.


Aina mbalimbali za ng’ombe wa maziwa huwa na mahitaji tofauti, hivyo kiwango cha maandalizi yako ni muhimu sana. Unahitajika kufahamu kuwa, unalazimika kufikia mahitaji yako kwa ajili ya lishe, si kwenye mahitaji ya awali tu bali pamoja na mahitaji ya baadaye ya ngo’mbe wako. Suala hili limefanya wafugaji wengi kushindwa kuendelea kutokana na kuwa hujiingiza katika shughuli hii bila kuangalia mambo ya msingi yanayotakiwa pamoja na kuweka mipango thabiti.


Pamoja na kuwa mahitaji yote kwa ajili ya lishe na mambo mengine yako sawa, ng’ombe wa maziwa ni lazima kuzalisha kulingana na umbile lake na uwezo wake kamili. Kama utaweza kumudu kufuga ng’ombe halisi wa maziwa, ni lazima pia utambue kuwa uzalishaji wa juu wa maziwa uhitaji pia usimamizi wa hali ya juu. Kwa maana hiyo, ni vyema kufuga ng’ombe wa kiwango cha kawaida (ikiwezekana chotara) ambaye ataendana na uwezo wako wa kumtunza.


Ni vyema tukaangalia aina mbili za ng’ombe wa maziwa ambao wana uwezo wa kuzalisha maziwa mengi;



Dairy cow - Copy
Ng’ombe aina ya Freshiani (Friesian)
(i) Freshiani (Friesian)



Ng’ombe aina ya freshiani ni rahisi kumtambua kutokana na kuwa na rangi nyeusi na nyeupe, na ni ng’ombe wenye uzalishaji bora wa maziwa. Wanyama hawa ni wakubwa na pia wanaweza kuwa na mabaka meupe na meusi au mekundu na meupe. Ikiwa watalishwa vizuri, freshian aliyefikia umri wa kukomaa huwa na uzito wa hadi kilogramu 550 na urefu wa sentimeta 150 kutoka begani. Mtamba huweza kupandwa, akiwa na umri wa miezi mitano huku akiwa na uzito wa kilogramu 360.


Wakati baadhi ya ng’ombe wakiwa na uwezo wa kuishi kwa muda mrefu, uwezo wa kawaida wa kuishi kwa Freshiani ni miaka sita. Hata hivyo, aina hii ya ng’ombe ni wazalishaji wazuri wa maziwa ambao huweza kuzalisha kilogramu 7800 kwa wastani kwa muda wa siku 360 yakiwa na kiwango cha chini cha mafuta ikilinganishwa na aina nyingine ya ng’ombe.


Aidha, aina hii ya ng’ombe huhitaji ulishaji mkubwa hivyo hushauriwa kwa wafugaji wenye uhakika wa kuwa na lishe bora na ya kutosha kwa mwaka mzima.


aysher
Ng’ombe aina ya Ayrshire
(ii) Ayrshire


Aina hii ng’ombe huwa na miraba ya kahawia na nyeupe karibu sawa na aina nyingine ya ng’ombe ambao huelekea kuwa na rangi ya (Mahogany). Ng’ombe hawa huwa na wastani wa kawaida, na uzito wa kilogramu 540 katika umri wa ukomavu. Aidha, humudu aina yeyote ya ufugaji na si rahisi kupata matatizo yeyote ya miguu.


Ayrshire huweza kufanya vizuri katika malisho ya aina yeyote tofauti na aina nyingine ya ng’ombe wa maziwa. Kukiwa na usimamizi mzuri na ulishaji mzuri, wastani wa uzalishaji wa maziwa ni kilogramu 5400 ikiwa na kiwango cha juu cha mafuta ukilinganisha na Freshian. Aryshire ni aina nzuri kwa kufuga hasa kutokana na nguvu aliyonayo pamoja na uzalishaji mkubwa wa maziwa. Ng’ombe wa aina hii, hutambulika kwa kuwa na umbo zuri pamoja na chuchu zake kuonekana kuwa zenye ubora. Aidha, utungaji wa maziwa yake, umefanya maziwa yake kuonekana ni mazuri sana katika uzalishaji wa siagi na jibini.


Maziwa ya Ayrshire yanafahamika kama “maziwa bora ya kunywa” kutokana na uwezo wake wa kuwa na mafuta ya kutosha na kiasi kikubwa cha protini. Kwa mfugaji anayeanza, aina hii ya ng’ombe ni nzuri sana kuanza nayo kasha baadaye kuongeza freshiani baada ya uwezo wako wa kuhudumia kuwa imara. Mifugo ya asili ni ghali sana na ni ngumu pia kuwapata, hivyo basi, njia rahisi kwa wafugaji wa maziwa wanaoanza ni kutafuta ng’ombe bora wa kawaida ambao mara nyingi huwa ni chotara, kisha kuwaboresha kwa kutumia mbinu ya kupandikiza dume bora na mwenye uzalishaji mkubwa. Na hii huhitaji elimu ya kutosha kuhusu uchaguzi wa madume.


*Muhimu: Wakati wa kununua ng’ombe kwa ajili ya kufuga, ni vyema mfugaji ukatambua kuwa, wazalishaji wa maziwa mara nyingi hawauzi ng’ombe wao wenye uzalishaji mzuri, badala yake huuza wale ambao hawazalishi kwa kiwango kizuri, wale wenye matatizo kama kutokushika mimba, wenye matatizo ya joto na wale ambao hushambuliwa na magonjwa mara kwa mara. Kwa maana hiyo, pamoja na aina ya ng’ombe unayehitaji kununua, ni muhimu sana kuwa mwangalifu usije ukanunua ng’ombe mwenye shida yoyote kwani hapo ndipo mwanzo wa uzalishaji wako kuja kuwa wa matatizo na kutokufikia lengo.

MIPANGO KATIKA UFUGAJI WA NG'OMBE WA MAZIWA

MIPANGO KATIKA UFUGAJI WA NG'OMBE WA MAZIWA

Mipango thabiti huleta mafanikio katika ufugaji wa ng’ombe wa maziwa. Wafugaji waliofanikiwa wanafahamu fika kuwa katika uzalishaji wa maziwa 20% inatokana na aina ya ng’ombe na 80% matunzo.

Watu wengi ambao wanataka kuanzisha ufugaji wa ng’ombe, lakini hawajui ni wapi pa kuanzia. Kwa kawaida, wao wanaweka pesa, kutafuta ng’ombe, kununua na mwisho hupata ng’ombe. Hapo ndipo kuhangaika na kupata msongo wa mawazo kwa mfugaji huanza kwa kuwa ng’ombe hazalishi maziwa kutokana na aina yake pekee.
Kwa wafugaji wadogo walio wengi, wakati ambapo ng’ombe anafika zizini kwake wanakuwa bado hawajawa tayari kumpokea ng’ombe huyo kwa ajili ya ufugaji. Ili ujasiria mali kwa njia ya ng’ombe uweze kufanikiwa na kumfaidisha mfugaji kiuchumi, mfugaji ni lazima ahakikishe kuwa miundo mbinu muhimu inakuwa tayari kabla ya kumleta ng’ombe.

N2 Mafanikio katika ufugaji wa ng’ombe wa maziwa huletwa na mipango mizuri

Kwa mujibu wa mwongozi wa kitabu cha ufugaji wa ng’ombe wa maziwa Afrika ya mashariki, ng’ombe wa maziwa ni lazima wapate mahitaji yafuatayo:
  • Malisho bora na maji safi ya kunywa
  • Afya bora bila majeraha
  • Mazingira safi ikiwa ni pamoja na  banda lililojengwa vizuri
  • Uangalizi mzuri na wa kirafiki,  ambao humfanya ng’ombe kuwa mtulivu bila kuwa na msongo.
Bila mahitaji haya muhimu, na mfugaji kutokumtunza ng’ombe vizuri, asitegemee kuwa ng’ombe huyo atazalisha kiwango kizuri cha maziwa. Uzalishaji wa kiwango cha maziwa na ubora wake unategemeana kwa kiasi kikubwa na mambo hayo yaliyotajwa hapo juu. Wataalamu wanasema kuwa 20% ya uzalishaji wa ng’ombe inatokana na aina ya ng’ombe na 80% matunzo kutoka kwa mfugaji. Muhudumie ng’ombe wako vizuri naye atarudisha kwa kuzalisha maziwa vizuri.

N3 Mafanikio katika ufugaji wa ng’ombe wa maziwa huletwa na mipango mizuri

Mipango

Wafugaji ni lazima wawe na mipango thabiti kwa ajili ya ufugaji wa ng’ombe. Hii hujumuisha idadi ya ng’ombe mfugaji anayotaka kufuga, pamoja na kufahamu ni kiasi gani cha malisho kinachohitajika kwa kipindi chote cha mwaka. Mfugaji pia anapaswa kufahamu kuwa ni kwa namna gani malisho yanafaa kutolewa kwa wanyama.
Mfugaji ni lazima pia apange ni kwa namna gani atapata malisho kwa kipindi chote. Hii inamaanisha kuwa ni muda gani atapanda, kuvuna na kuhifadhi. Mipango ni nguzo muhimu sana kwa kuwa inawezesha kusaidia kufahamu ni nini cha kufanya, namna ya kufikia malengo yaliyokusudiwa, na ni hatua gani imefikiwa. Mfugaji ambaye hana mipango thabiti ni sawa na mtu anayeanza safari bila kufahamu mwisho wa safari yake ni wapi.

Mahitaji ya mlo kamili

Shughuli ya ufugaji wako itakamalika siku ambayo utaweza kuelewa uhusiano kati ya ulishaji wa ng’ombe, uzalishaji wa maziwa na mapato. Endapo ng’ombe wa maziwa atalishwa kwa malisho hafifu ni dhahiri kuwa uzalishaji wa maziwa pia utakuwa hafifu.

Malisho bora

Tafuta ni aina gani ya malisho hufanya vizuri katika ukanda wako. Malisho endelevu hutegemeana kwa kiasi kikubwa na aina ya malisho na utunzaji wake shambani mwako. Chukulia kuwa wewe ni mfugaji mdogo na hauwezi kumudu gharama za umwagiliaji, ni lazima utumie kwa kiasi kikubwa malisho ya wakati wa mvua na kuhifadhi ili kuweza kuyatumia wakati wa kiangazi.
Inashauriwa kupanda majani ya malisho kwa kiasi kikubwa uwezavyo wakati wa mvua. Wahamasishe majirani zako kupanda malisho pia, ili baadaye uweze kununua kutoka kwao. Matete, nyasi, majani ya mtama, majani ya mahindi, lusina, desmodiamu, na alizeti ni miongoni mwa malisho ambayo hufanya vizuri katika maeneo mengi nchini Tanzania.

Kiwango cha kutosha

Fahamu ni kiwango gani kinachotosha kwa kila ng’ombe wako. Hii itakusaidia kufahamu ni kiasi gani cha malisho upande na ni kiasi gani uhifadhi. Kwa wastani, ngombe wa maziwa aliyekomaa mwenye uzito wa kilo 400, anayefugwa ndani ana uwezo wa kula kilo 12 za majani makavu kwa siku. Kumbuka kuwa endapo mifugo yako haitapata malisho ya kutosha wataonesha kwa muonekana wao, na kisha kukupa adhabu kwa kuzalisha maziwa kidogo sana. Kama kanuni inavyoeleza, hakikisha kuwa 15%-18% ya malisho yote ni protini.

Zingatia utunzaji na uzalishaji wa malisho vizuri

Wafugaji walio wengi hukwepa kupanda majani ya malisho kwa kuogopa gharama ya mbolea na mbegu. Kwa uzoefu wetu mfugaji anaweza kutumia mbolea inayotokana na wanyama kupanda malisho na kuyatunza vizuri. Matete ni moja wapo ya malisho hayo. Endapo malisho hayo yatawekwa mbolea vizuri, shamba dogo tu la malisho linaweza kukupatia malisho ya mifugo kwa kipindi chote cha mwaka.

Weka malisho katika hali ya usafi

Hifadhi malisho katika sehemu nzuri, sehemu ambayo hayatapigwa na jua moja kwa moja, mvua au kuwepo uwezekano wa vitu vingine vinavyoweza kuyaharibu kama vile siafu na wadudu wengineo. Majani ya malisho ni lazima yanyaushwe vizuri kuepuka viini vya sumu vinavyoweza kuwepo kwenye malisho. Mfugaji anaweza kuamua juu ya ubora wa malisho kutokana na muonekano wake, harufu na mguso. Malisho mabichi yenye wingi wa majani kuliko shina, yenye kijani kilichokolea, na ambayo yana mguso nyororo, ni moja ya malisho bora ukilinganisha na yale yenye ugumu, shina kubwa na rangi ya njano. Epuka kulisha mifugo yako kwa kutumia malisho yenye ukungu kwa kuwa yanaweza kuwa na sumu.

Kuweka kumbukumbu ni muhimu

Uwekaji wa kumbukumbu ni muhimu lakini huwa hauzingatiwi na wafugaji walio wengi. Baadhi ya wafugaji huona kama uwekaji wa kumbukumbu ni kazi ya ziada, ambayo kulingana na wao haina uhusiano wowote na mapato yanayotokana na shughuli zao. Hata hivyo, bila uwekaji sahihi wa kumbukumbu, mfugaji hawezi kufahamu ni mapato kiasi gani anayopata kutokana na shughuli ya ufugaji. Ni kwa namna gani mfugaji anaweza kufahamu wakati wa kumpandisha ng’ombe wake, kama hajui kuwa zimepita siku ngapi tangu ng’ombe huyo alipozaa!

N4 Mafanikio katika ufugaji wa ng’ombe wa maziwa huletwa na mipango mizuri

MABANDA YAKUFUGIA NG'OMBE WA MAZIWA

 MABANDA YAKUFUGIA NG'OMBE WA MAZIWA


Kabla mfugaji hajafikiria kuhusu makazi ya ng’ombe wake, ni vyema sana kujiuliza ni kiasi gani cha mifugo utahitaji kuwa nao baada ya miaka kadhaa hivyo kukuwezesha kutenga nafasi ya kutosha kwa ajili ya mifugo utakayoleta.


Njia rahisi ya kulitambua hilo, ni kujiuliza ni kiasi gani cha mifugo ungependa kuwa nao baadaye na ni kiwango gani cha uzalishaji wa maziwa ungetarajia kufikisha kutoka kwa ng’ombe wako.


banda smart.PG - Copy

Swali la kwanza, ni muhimu sana kwa mfugaji kujiuliza, kwani kiwango cha mifugo hutokana na uwezo wa kiwango cha lishe utakachohitajika kulisha mara kwa mara. Kwa kawaida, ekari moja ya ardhi hutoshea kulisha ng’ombe wa maziwa aina ya Freshiani mmoja au Jesrey wawili tu.


Ng’ombe wa maziwa mmoja (Fresian, Guernsey, Jersey) kiasi cha tani 5 ya lishe ya majani mabichi au majani makavu kwa mwaka. Hii ni sawa na kilogramu 25,000 za matete au kiasi cha majani uliyoyaotesha kwenye ekari moja. Pamoja na usimamizi mzuri wa malisho ya nyasi, au mchanganyiko wa malisho kama mikunde au mimea kama desmodium, ni dhahiri kuwa bado utahitajika kuwa na angalau ekari ya ziada 0.75 ya eneo ili kuweza kulisha ng’ombe wako vizuri.


Kwa ujumla, ng’ombe wa maziwa huhitaji lishe kiwango kikubwa kuliko ng’ombe wa nyama, na mara nyingi huwa na uzalishaji mkubwa pale ambapo ubora wa lishe ni wa hali ya juu. Hali kadhalika, kama utazalisha malisho yako mwenyewe, bado utahitaji njia nyingine ya ziada ya kupata lishe ikiwa itatokea tatizo lolote katika malisho.


Jedwahi hili huonesha kiwango cha lishe kinachohitajika kwa aina mbalimbali ya ng’ombe wa maziwa, pamoja na ardhi kwa ajili ya kuzalishia malisho.

Jedwali



Ufugaji wa ndani



Katika ufugaji wa ndani, ng’ombe wanahitajika kuwekwa kwenye hali ya usafi, na makazi yao yawe na ulinzi wa kutosha na yenye kuwapatia uhuru. Wafugaji walio wengi wamekuwa wakiwekeza fedha nyingi katika kuwajengea mifugo, na mwishoni kuishia
kukosa fedha kwa ajili ya kulishia mifugo hiyo. Mfugaji anayeanza, anashauriwa kujengea mifugo yake makazi mazuri na ya gharama nafuu na baadaye kuendeleza mabanda hayo kutokana na mapato yanayopatikana.


Mambo ya kuzingatia katika ujenzi wa mabanda



Nafasi: Ng’ombe mkubwa anahitaji kuwa na nafasi ya kutosha kwa ajili ya chakula, kupumzika pamoja kufanya mazoezi jambo ambalo wafugaji walio wengi hawazingatii na badala yake huweka mifugo yao katika nafasi ndogo ambayo mwishoni hudidimiza ukuaji wa mnyama na uzalishaji kwa ujumla. Kwa mantiki hiyo, ng’ombe mmoja mkubwa anahitaji mita za mraba 8 mbali na eneo lake la kupumzikia. Njia rahisi ni kutenga eneo hili mbele ya zizi/banda. Kumbuka, unapokuwa na nafasi kubwa, ndipo unapotengeneza uzalishaji mzuri.


Paa: Ni vyema kukawa na paa kwa ajili ya kuilinda mifugo dhidi ya upepo, mvua pamoja na jua kali. Hakikisha paa linakuwa juu, ili kuipa uhuru mifugo yako kutembea ndani ya banda bila tatizo lolote. Hakikisha mteremko wa paa hauwezi kuathiri sehemu ya mifugo kupumzika na sehemu ya lishe hasa kwa kuruhusu maji kuingia katika sehemu hizo.


cow beddings - Copy

Ni muhimu ng’ombe kuwa na mahali safi pa kulala

Sakafu: Hakikisha sakafu inakuwa na mfumo mzuri wa mifereji kwa ajili ya kuruhusu maji na mkojo kupita hivyo kuwaweka mifugo katika hali nzuri. Unaweza kutengeneza sakafu ya simenti ambayo ni rahisi kusafisha. Hata hivyo kwa kuwa inagharimu fedha, mfugaji anaeanza, anaweza kutumia udongo wa mfinyanzi au aina nyingine ya udongo mgumu kutengeneza sakafu. Endapo utasakafu banda, sakafu isiwe inayoteleza kwa kuwa ng’ombe wanaweza kuteleza na kuumia. Sakafu iwe na mwinuko kidogo na mwinuko uelekee sehemu ya kutiririshia mkojo na kutolea kinyesi.


Matandiko: Eneo ambalo mifugo hupumzikia, ni vyema kukawa na matandiko. Unaweza kutumia malighafi ya aina yeyote kavu ambayo huweza kunyonya mkojo na samadi. Matandiko hayo ni lazima kubadilishwa mara kwa mara.



Vihondi vya maji na chakula: Hakikisha kuna vihondi vya kutosha kwa ajili ya chakula na maji. Mabanda ni vyema yakawa karibu na vyanzo vya upatikanaji wa maji safi na salama. Kwa wastani, ng’ombe mmoja anahitaji kunywa maji kiasi cha lita kati ya 50 au 80 kwa siku sawa na ndoo 5 hadi 8 za maji (za ujazo wa lita 10).


Shimo la mbolea: Mifugo inayolishwa vizuri hutoa samadi nyingi hivyo huweza kuwa tatizo kwa watu wanaokuzunguka hasa ikiwa inatapakaa kila mahali na kusababisha kuwepo kwa harufu mbaya. Kama utafuga mifugo mingi katika eneo dogo bila kuwa na sehemu maalumu ya kuweka mbolea inayotokana na mifugo hiyo, basi ni dhahiri kuwa utasababisha kutokuelewana na majirani, lakini pia kutasababishia wanyama kukaa katika hali ya usumbufu. Ni vyema kuandaa shimo maalumu kwa ajili ya samadi hasa kwa ufugaji wa ndani, kabla ya kutumia kwa ajili ya kuweka kwenye mashamba ya malisho.

UFUGAJI WA NG'OMBE KENYA

Ufugaji wa ng'ombe Kenya

Ufugaji wa ng’ombe barani Afrika hukimu riziki ya idadi kubwa haswa wale wanaoishi katika sehemu kame. Ngo’mbe hufugwa kwa ajili ya nyama na maziwa na kwa manufaa mengine kama ngozi, katika kazi ya utayarishaji wa ardhi na usafiri na uzalishaji wa mbolea.

Ufugaji wa ng’ombe kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa ni biashara inayotuza sana na katika nchi ambazo mpangilio mzuri hufuatwa, makampuni na watu binafsi wanatengeneza mapato ya juu. Misri, Sudan, Afrika Kusini na Kenya ni baadhi ya nchi barani Afrika ambazo zina biashara inayofana katika bidhaa za ng’ombe.

Katika nchi kama Kenya, 80% ya maziwa inazalishwa na wakulima wadogo wadogo wapatao elfu 600,000 ilhali nchini Afrika Kusini soko linatawaliwa na wakulima wakubwa wakubwa wapatao elfu 4,000.

Ingawaje Kenya huzalisha maziwa mengi kuliko Afrika Kusini, hupata mapato machache. Ukilinganisha, Kenya ilizalisha lita bilioni elfu 3.5 za maziwa katika mwaka wa 2006 na ikapata shilingi za Kenya ziipatazo bilioni 64 ilhali Afrika Kusini ilizalisha lita bilioni 2.6 na kupata shilingi za Kenya zipatazo Bilioni 220.

Kwa nini? Ni kwa sababu mengi ya maziwa nchini Kenya hutumiwa bila ya kutayarishwa ilhali nchini Afrika Kusini maziwa hutayarishwa kutengeneza bidhaa zenye thamani ambazo zinauza zaidi na hudumu kwa mda mrefu.

Hii inaonyesha ukulima wa kufuga ng’ombe kwa ajili ya maziwa una uwezekano mkubwa lakini ikiwa tu utasimamiwa vizuri kwa uzalishaji mzuri, lishe bora kwa wanyama na usimamizi mzuri wa biashara ya kufuga ng'ombe.

Katika sehemu hii, jifunze zaidi kuhusu;

  • Vizazi vya ng’ombe
  • Uzalishaji na usimamizi wa ng’ombe wako
  • Utengenezaji wa rekodi za ng’ombe
  • Giving Birth and Caring for the Calf
  • Kujifungua na kumtunza ndama
  • Ukamaji na kusimamia ukamaji
  • Lishe ya ng’ombe na mbinu za ulishaji
  • Magonjwa ya ng’ombe
  • Bidhaa za ng’ombe

KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA NG’OMBE WA MAZIWA


KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA NG’OMBE

Ng’ombe wanafugwa kwa ajili ya nyama na maziwa lakini pia hutoa mazao mengine kama ngozi,mbolea na hutumika kama wangyama kazi.  Zaidi ya asilimia95 ya ng,ombe na hutumika kama wanyama kazi.  Zaidi ya asilimia 95 ya ng’ombe wanaofugwa hapa nchini ni wa asili ambao huzalisha nyama na maziwa kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na wale wachache walioboreshwa.  Ng’ombe walioboreshwa wamegawanyika katika makundi mawili, wale wanaofugwa kwa ajili ya nyama na wanaofugwa kwa ajili ya maziwa.  Ili kuwawezesha ng’ombe kuzalisha mazao bora ya nyama, maziwa na ngozi mfugaji anapaswa kufuata kanuni za ufugaji bora ambazo ni pamoja na:-
 
i)                  Kufuga ng’ombe katika eneo kwa kuzingatia uwianao wa idadi ya ng’ombe na malisho katika mfumo wa      ufugaji huria.
ii)                  Kujenga banda au zizi bora.
iii)                 Kuchagua koo/aina ya ng’ombe kulingana na uzalishaji (nyama au maziwa).
iv)                  Kutunza makundi  mbalimbali ya ng’ombe kulinga na umri na hatua ya uzalishaji.
v)                   Kumpa ng’ombe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili.
vi)                  Kudhibiti magonjwa ya ng’ombe kama inavyoshauriwa na mtaalamu wa mifguo.
vii)                Kuvuna mifugo katika umri na uzito muafaka kulingana na mahitaji ya soko.
viii)               Kuzalisha maziwa, nyama na ngozi zinazokidhi viwango vya ubora na usalama.
ix)                  Kutunza kumbukumbu za uzalishaji na matukio muhimu ya ufugaji.
MIFUMO YA UFUGAJI
Ng’ombe wanaweza kufugwa katika mfumo wa ufugaji huria au kulishwa katika banda (ufugaji shadidi).  Ufugaji huria huhitaji eneo kubwa la ardhi yenye malisho mazuri na vyanzo vya maji.  Pamoja na kuwa na ufugaji huu, ni muhimu ardhi hiyo itunzwe kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya ng’ombe na malisho.  Ufugaji wa shadidi uzingatie uwepo wa banda bora na lishe sahihi.
UFUGAJI KATIKA MFUMO HURIA
Ili mfugaji aweze kupata mazao mengi na bora katika ufugaji huria anapaswa kuzingatia yafuatayo:-
-           Atenge eneo la kutosha la kufugia kulingana na idadi ya ng’ombe alionao.
-          Atunze malisho ili yawe endelevu na yapatikana wakati wote.
-          Awe na eneo lenye maji ya kutosha na
-          Atenganishe madume na majike ili kuzuia ng’ombe kuzaa bila mpangilio.
Matunzo mengine ya ng’ombe yazingatie vigezo vingine muhimu kama umri hatua ya uzalishaji na matumizi ya ng’ombe husika.
BANDA/ZIZI BORA LA NG’OMBE
BANDA BORA.
Band alijengwe sehemu ya mwinuko mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa zifuatazo:-
·         Uwezo wa kumkinga ng’ombe dhidi ya mvua, upepo, jua kali na baridi.
·         Kuta imara zenye matunda au madirisha kwa ajili ya kuingiza hewa na mwanga wa kutosha,
·         Sakafu yenye mwinuko upande mmoja ili isiruhusu maji na uchafu kutuama.
·         Lijengwe katika hali ya kuruhusu kufanyiwa usafi kwa urahisi kila siku, na sakafu ngumu ya zege au udongo ulioshindiliwa na kuweka malalo.
·         Paa lisilovuja na
Aidha kwa wafugaji wanaofuga katika ufugaji huria ambako mazizi hutumika, inashauriwa  kuzingatia yafuatayo:-
·         Zizi likae mahali pa mwinuko pasiporuhusu maji kutuama.
·         Zizi liweze kukinga mifugo dhidi ya wezi na wanyama hatari.
·         Ukubwa wa zizi uzingatie idadi na umri wa mifugo ng’ombe watengwe kulingana na umri wao.
·         Zizi lifanyiwe usafi  mara kwa mara na
·         Liwe na sehemu ya kukamulia (kwa ng’ombe wa maziwa), stoo ya vyakula, sehemu ya kutolea huduma za kinga na tiba, eneo la kulishia na maji ya kunywa.
ZIZI BORA 
Zizi lijengwe sehemu ya mwinuko isiyoruhusu maji kutuama mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa zifuatazo:-
§  Liweze kuhakikisha usalama wa ng’ombe.
§  Ukubwa wa zizi uzingatie idadi ya mifugo.
§  Liwe na sakafu ya udongo ulioshindiliwa vizuri na kufanyiwa usafi  mara kwa mara
§  Zizi la ndama liwe na paa ma
§  Lijengwe kwa vifaa madhubuti na visivyoharibu ngozi.
UCHAGUZI WA KOO NA AINA YA NG’OMBE WA KUFUGA
Kwa ufugaji wenye tija, mfugaji anashauriwa kuchagua koo na aina ya ng’ombe kwa kuzingatia malengo ya ufugaji (nyama au maziwa).
NG’OMBE WA NYAMA
Ng’ombe wanaofaa kufugwa kwa ajili ya uzalishaji nyama ni wale wanaokua kwa haraka na kuweka misuli mikubwa iliyojengeka vizuri.  Baadhi ya koo zenye sifa hizo ni pamoja na Boran, Mpwapwa (nyama na maziwa), Charolais, Aberdeen Angus, pamoja na chotara wao.  Hata hivyo, nchini Tanzania ng’ombe aina ya Zebu (mfano Ufipa,Gofo, Masai, Sukuma, Tarime, Iringa red), Sanga (Ankole) na chotara wao ndio hutumika kama ng’ombe.
NG’OMBE WA MAZIWA.
Sifa za ng’ombe wa maziwa zifuatazo:-
-           Umbo lililopanuka kwa nyuma na kupungua kuelekea kichwani.
-          Mgongo ulionyooka kuanzia mabegani kuelekea mkiani
-          Miguu ya nyuma mirefu iliyonyooka, minene yenye kuacha nafasi kwa ajili ya kiwele na kwato imara.
-          Kiwele kiwe kikubwa chenye chuchu nne, ndefu na unene wa wastani
-          Nafasi kati ya chuchu na chuchu iwe ya kutosha na
-          Endapo ng’ombe anakamuliwa awe na kiwele kikubwa kilichoshikamana vizuri mwilini, na mishipa mikubwa kwenye kiwele iliyosambaa.
Aina ya ng’ombe wa maziwa wanaofugwa kwa wingi nchini ni pamoja na Friesian, Ayrshire, jersey, Mpwapwa, Simmental na chotara watokanao na mchangoayiko wa aina hizo na Zebu.
UTUNZAJI WA MAKUNDI MABALIMBALI YA NG’OMBE WA MAZIWA KULINGANA NA UMRI NA HATUA YA UZALISHAJI
UTUNZAJI WA NDAMA
Mfugaji anapaswa kutunza ndama vizuri kwa lengo la kupata ng’ombe wengi na bora kwa ajili ya maziwa.  Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ndama tangu kuzaliwa hadi kuachishwa maziwa ni pamoja na
-           Kuhakikisha kuwa ndama anapakwa dawa ya kuzuia maambukizi ya viini ya magonjwa kupitia kwenye kitovu, kwa mfano dawa joto (Tincute of Iodine) mara baada ya kuzaliwa na
-          Ndama apatiwe maziwa ya awali yaani dang’a (colostrums) mara baada ya kuzaliwa kwa lengo la kupata kinga ya mwili dhidi ya magonjwa.  Aidha, aendelee kunyonya maziwa hayo kwa muda wa siku 3-4.
Endapo jike aliyezaa amekufa au hatoi maziwa, apewe dang’a toka kwa ng’ombe mwingine kama yupo au dang’a mbadala, ambayo inaweza kutengenezwa kwa kuchanganya vitu vifuatavyo:-
-           Lita moja ya maziwa yaliyokamuliwa wakati huohuo.
-          Lita moja ya maji yaliyochemshwa na kupozwa hadi kufikia joto la mwili.
-          Kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya samaki (cod liver oili).
-          Mafuta ya nyonyo vijiko vya chai 3 na
-          Yai moja bichi
Koroga mchanganyiko huo, weka katika chupa safi na ndama anyweshwe kabla haujaopoa.  Ndama anyweshwe mchanganyiko huo mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 3 mfululizo na kila mara mchanganyiko uwe mpya.  Wakati wa kunywesha chupa iwekwe juu ya  kidogo ili asipaliwe.
-           Endapo ndama hawezi kunyonya ng’o mbe akamuliwe na ndama anyweshwe maziwa kwa njia ya chupa kwa kuzingatia usafi wa maziwa na chupa.
-          Ndama aendelee kunyweshwa maziwa kwa kiasi kama ilivyoonyeshwa kwenye Jedwali Na. 1
-          Ndama aanze kuzoeshwa kula nyasi laini, pumba kidogo na maji safi wakti wote kuanzia wiki ya 2 baada ya kuzaliwa na
-          Ndama aachishwe kunyonya au kupewa maziwa akiwa na umri wa miezi 3.  Mfugaji ahakikishe kwamba ndama anayeachishwa kunyonya ana afya nzuri.
JEDWALI NA. 1 KIASI CHA MAZIWA NA CHAKULA MAALUMU KWA NDAMA
UMRI (WIKI)
KIASI CHA MAZIWA KWA SIKU (LITA)
KIASI CHA CHAKULA MAALUM CHA NDAMA KWA SIKU (KILO)
1
3.0
0.0
2
3.5
0.0
3
4.0
0.0
4
4.5
0.0
5
5.0
0.1
6
5.0
0.2
7
5.0
0.3
8
4.0
0.4
9
3.0
0.7
10
2.0
1.0
11
1.5
1.25
12 - 16
0.75
1.5
Vyombo vinavyotumika kulishia ndama visafishwe vizuri kwa maji yaliyochemshwa, sabuni na kukaushwa.
Matunzo mengine ya ndani ni pamoja na:-
-           Kuondoa pembe kati ya siku 3 hadi 14 mara zinapojitokeza ili kuzuia wanyama kuumizana na kuharibu ngozi,
-          Kukata chuchu za ziada kwa ndama jike
-          Kuhasi ndama dume wasiozidi umri wa miezi 3 ambao hawatahitajika kwa ajili kuendeleza kizazi ili wakue hawatajika kwa ajili ya kuendelea kizazi ili wakue haraka na kuwa na nyama nzuri.
-          Kuweka alama au namba za utambulisho kati ya siku ya kwanza na ya tano, mfano kuvalishwa hereni kwenye masikio kwa ajili ya urahisi wa udhiti wa umiliki na utunzaji kumkukumbu na,
-          Kuwapatia kinga dhidi ya maabukizi na tiba ya magonjwa wanapougua.
Huduma hizi zifanyike chini ya maelekezo ya mtaalam wa mifugo.
UTUNZAJI WA NDAMA BAADA YA KUACHISHWA MAZIWA HADI KUPEVUKA (MIEZI – 18)
-           Ndama baada ya kuachishwa maziwa apate malisho bora na chakula mchanganyiko kuanzia kilo 2 4 kwa siku kutegemea umri wake na
-          Ndama wanapofikia umri wa miezi 18 wachaguliwe wanaofaa kuendeleza kizazi, wasio na sifa nzuri waondolewe katika kundi
.
UTUNZAJI WA MTAMBA
Mtamba ni ng’ombe jike aliyefisha umri wa kupandwa (wastani wa miezi 18) hadi anapozaa kwa mara ya kwanza.  Ni muhimu kutunza vizuri mtamba ili kupata kundi bora la ng’ombe.  Miezi 3 kabla ya kupandishwa mtamba apatiwe:-
-           Malisho bora
-          Maji ya kutosha
-          Madini  mchanganyiko na
-          Chakula cha ziada kiasi cha kilo 2 – 3 kwa siku, ili kuchochea upevukaji na kuongeza uzito wa mwili.
UTUNZAJI WA NG’OMBE WAKUBWA
Kundi hili linajumuisha ng’ombe wenye mimba, wanaokamuliwa na madume.  Mfugaji anapaswa kutunza vizuri ng’omb